FG

PAGES

WANAFUNZI WA SHAHADA YA KWANZA YA SOSHOLOJIA YA CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM) WAPOKEA MWAKA KWA UPANDAJI WA MITI MKOA

 Baadhi ya wanafunzi wa shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) wakisikiliza kwa makini wakati wakipewa elimu ya mazingira wakati walipoenda kupanda miti katika Shule zilizopo Mjini Dodoma
 Mmoja wa Wanafunzi wa shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Dorry Michael akipanda mti katika Shule ya Sekondari ya Itenga iliyopo Nkuhungu Mjini Dodoma
 Wanafunzi wa Shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) wakiwa wanapanda Miti katika Shule ya Sekondari ya Itenga iliyopo Nkuhungu,Wilaya ya Dodoma Mjini Mkoani Dodoma
 Wanafunzi wa Shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) wakipanda miti katika Shule ya Sekondari ya Itenga iliyopo Nkuhungu wilaya ya Dodoma Mjini Mkoani Dodoma
Baadhi ya wanafunzi wa Shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) wakiwa katika Picha ya Pamoja na mratibu wa elimu wilaya ya Dodoma Mjini mara baada ya Kumaliza zoezi la upandaji wa Miti katika Shule ya Sekondari Itega iliyopo Nkuhungu, Wilaya ya Dodoma Mjini, Mkoani Dodoma

WANAFUNZI WA UDOM WAJITOLEA KUCHANGIA DAMU KWA HIARI LEO

Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma Prof Idris Kikula (Wa Pili Kushoto) akiwa amesimama wakati akimkaribisha mgeni rasmi ambaye ni  mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini Mh Lephy Gembe aliyeongozana na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa Wa Dodoma, Na Balozi Job Lusinde katika zoezi la kujitolea damu kwa hiari lililofanyika siku ya leo Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) na Kuandaliwa na Taasisi ya Wanafunzi wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO)
Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Prof Idris Kikula akitoa neno la ukaribisho kwa Mgeni Rasmi na timu yake nzima wakati walikuja kufungua zoezi la kujitolea damu kwa hiari kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) zoezi lililoandaliwa na Taasisi ya Wanafunzi wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOMSSO) zoezi lililofanyika leo Chuoni Hapo
Mgeni Rasmi ambaye pia ni Mkuu Wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mh Lephy Gembe akitoa neno fupi kwa wanafunzi na wafanyakazi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma waliofika katika Zoezi la Kujitolea Damu kwa Hiari lililofanyika Chuo Kikuu Cha Dodoma leo.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa wamejitokeza katika zoezi la kuchangia Damu kwa hiari lililofanyika leo Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOM) na kuandaliwa na taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOM)
Afisa Mahusiano wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Bi Beatrice alipokua akitoa damu kwa hiari katika Zoezi la Kuchangia Damu kwa Hiari lililofanyika Chuo Kikuu Cha Dodoma leo huku Akishuhudiwa na Mshauri wa wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Mh Manongi(Mwenye Miwani)
Baadhi ya Viongozi wa taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOMSSO) ambao Pia Wamemaliza Muda wao rasmi leo Wakiwa katika zoezi la Uchangiaji Hiari wa Damu zoezi lililofanyika Chuo Kikuu Cha Dodoma leo ambalo liliandaliwa na Taasisi ya wanafunzi wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Sosoholojia Ya Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOMSSO). Kutoka Kushoto Ni Emmanuel Mwakibinga akifuatiwa na Stefano Saimon.
Afisa habari wa Taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya sosoholojia aliyemaliza rasmi muda wake leo ambaye pia ni Mmiliki wa Mtandao wa LUKAZA BLOG Mh Josephat Lukaza akiwa tayari ameshamaliza zoezi la uchangiaji wa Damu kwa Hiari ambalo liliandaliwa na taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO) zoezi lililofanyika leo Chuo Hapo.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma wakiwa Wanasubiri Kwenda Kutoa damu kwa hiari lililoandaliwa na taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOMSSO) zoezi lililofanyika Chuo Kikuu Cha Dodoma leo
Makamu Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Prof Idris Kikula akiaga wanafunzi na wafanyakazi waliojitoa katika zoezi la uchangiaji damu kwa hiari lililoandaliwa na taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO) lililofanyika chuo hapo leo

SHEREHE YA KUWAAGA WANAFUNZI WA MWAKA WA TATU WANAOSOMA SHAHADA YA KWANZA YASOSHOLOJIA YA UDOM YAFANA USIKU WA KUAMKIA LEO KATIKA UKUMBI WA VETA MJINI DODOMA

Mgeni rasmi ambaye pia ni Mkuu mpya wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mh Leph Gembe akiingia Ukumbini huku akisindikizwa na Mwenyekiti wa taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOMSSO) aliyemaliza muda wake Bw Emmanuel Misungwi katika ukumbi wa veta uliopo Mkoani Dodoma katika Sherehe ya kuwaaga mwaka wa tatu wanaosoma shahada ya kwanza ya sosholojia ya chuo kikuu cha Dodoma (UDOM)
Mgeni rasmi ambaye pia ni Mkuu Mpya wa Wilaya ya Dodoma Mjini (Wa Pili Kushoto)Mh Leph Gembe akiwa katika Picha ya Pamoja na baadhi ya Viongozi wa taasisi ya wanafunzi wanaosoma shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma(UDOMSSO) ambao wamemaliza muda wao ambapo wa kwanza kushoto ni Mwalimu mlezi wa taasisi hiyo Bw. Jeremiah katika sherehe ya Kuwaaga wanafunzi wa mwaka wa tatu wanaosoma shahada ya kwanza ya sosholojia
Baadhi ya wanafunzi wa mwaka wa tatu ambao wanasoma shahada ya kwanza ya sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma Wakiingia ukumbi kwa staili ya kucheza kwaito katika sherehe ya kuwaaga mwaka wa tatu iliyofanyika katika ukumbi wa veta uliopo dodoma mjini
Baadhi ya wanafunzi walioshiriki katika sherehe ya kuwaaga mwaka wa tatu iliyofanyika katika ukumbi wa veta uliopo mjini Dodoma
Mwenyekiti Wa Kwanza na Muasisi wa taasisi hii ya wanafunzi wanaosoma sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma ambaye amehitimu mwaka 2011 Mh Ibrahim Bakari akitoa neno wakati wa sherehe ya kuwaaga wanafunzi wa mwaka wa tatu katika sherehe iliyofanyika katika ukumbi wa veta
Makamu Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Bi Gaundensia Mwakemwa akimvalisha kitambulisho Makamu Mwenyekiti Mpya Bw Mtono Juma  kama ishara ya kukabidhi madaraka kwa viongozi wapya wa taasisi hiyo.
Mwenyekiti mpya wa taasisi ya wanafunzi wanaosoma sosholojia ya chuo kikuu cha Dodoma Bw Edgar Kelvin akimkabidhi zawadi mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini Mh Leph Gembe ambaye pia alikua mgeni rasmi wa sherehe ya kuwaaga wanafunzi wa mwaka wa tatu wanaosoma shahada ya kwanza ya sosholojia ya chuo kikuu cha Dodoma
Wadada safi kabisa wakiwa wamebeba keki tayari kwaajili ya kuikata
Wawakilishi wa wanafunzi walioitwa mbele kwaajili ya kukata keki kutoka kushoto  ni Mwanafunzi Loyce Haule, Katikati ni Shabani Kambi na Mwisho kabisa Ni Beatrice Msami
Baadhi ya wanafunzi wa mwaka wa tatu na viongozi waliomaliza muda wao wakipokea vyeti kutoka kwa mgeni rasmi ambaye pia ni Mkuu Mpya Wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mh Leph Gembe kama ishara ya kutambua majukumu yao kipindi wakiwa katika nafasi za uongozi
Muda wa Maakuli huo
 
MWENYEKITI WA KWANZA NA MUASISI WA UNIVERSITY OF DODOMA SOCIOLOGY STUDENTS ORGANIZATION(UDOMSSO) AMBAYE AMEHITIMU KATIKA CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOM) MWAKA 2011 NDUGU IBRAHIM BAKARI  (Wa kwanza Kushoto) KATIKA PICHA YA PAMOJA NA AFISA HABARI WA UDOMSSO ALIYEMALIZA MUDA WAKE JANA NDUGU JOSEPHAT LUKAZA KATIKA SHEREHE YA KUTUAGA MWAKA WA TATU TUNAOSOMA SHAHADA YA KWANZA YA SOSHOLOJIA YA CHUO KIKUU CHA DODOMA

TAASISI YA WANAFUNZI WANAOSOMA SHAHADA YA KWANZA YA SOSHOLOJIA YA CHUO KIKUU CHA DODOMA (UDOMSSO) YAPATA VIONGOZI WAPYA LEO MCHANA

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Kutoka Mwaka wa 1 alipokua akitoa maelekezo ya nini kifanyike kabla ya Zoezi la Kupiga kura na Kutangaza washindi
 Mgombea wa Nafasi ya Mwenyekiti katika taasisi ya wanafunzi wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO) Bw Edgar Kelvin ambaye anasomma mwaka wa 2 alipokua akinadi sera zake kabla zoezi la kupiga alijaanza
Mgombea wa pili wa nafasi ya Mwenyekiti katika taasisi ya Wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO) Bi Loyce Haule ambaye anasoma mwaka wa 2 akinadi Sera zake
Mgombea wa Tatu wa Nafasi ya Mwenyekiti katika taasisi ya Wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO) Bw Mwakindaga Emmanuel ambaye anasoma mwaka wa 2 akinadi sera zake
Mgombea Wa Nafasi ya Makamu Mwenyekiti katika taasisi ya Wanafunzi wanaosoma shahada ya kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO) Bw Mtono Juma ambaye amepita bila kupingwa kutoka na kuwa mgombea pekee wa nafasi hiyo na ni mwanafunzi kutoka mwaka wa kwanza
Mmoja wa Wanafunzi Kutoka Mwaka wa 3 Sophia Mkingiye akiuliza Maswala mara baada ya Wagombea kumaliza kunadi sera wakati walipokua wakiomba kura kwa wajumbe na wanachama
Mwanafunzi wa Mwaka wa 2 ambaye anasoma shahada ya kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma Bi Hadija Hassan alipokua akiuliza swali wakati kwa wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanafunzi wanaosoma shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma Wakati Wa Uchaguzi wa Kuwachagua Viongozi wapya wa Nafasi mbalimbali Katika Taasisi hiyo Mchana wa Leo
Baadhi ya wanafunzi wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma waliohudhuria katika uchaguzi wa kuchagua viongozi wa taasisi ya Wanafunzi wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO) katika uchaguzi uliofanyika ndani ya Chuo Kikuu Cha Dodoma mchana wa leo
Zoezi la Kuesabu kura likiendelea hapo 
Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Bw Emmanuel Misungwi Alipokua akitoa Shukrani wa wanachama na wadau wa taasisi hiyo Kwa Kipindi Chote alichokua madarakani kwa mazuri na mabaya ambayo taasisi imepitia na kushukuru kwa wanachama kushiriki zoezi la kupiga kura na kupata viongozi wapya wa Taasisi ya Wanafunzi wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOMSSO)
Baadhi ya Viongozi wapya wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi waliomaliza muda wao leo mara baada ya zoezi la kupiga kura kumalizika na hatimaye kuwapata viongozi wa taasisi ya wanafunzi wanasoma shahada ya kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma mchana wa leo
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanafunzi wanaosoma Shahada ya Kwanza ya Sosholojia ya Chuo Kikuu Cha Dodoma aliyemaliza muda wake leo Mh Emmanuel Misungwi (Katikati) Akiwa katika Picha ya Pamoja na Mwenyekiti mpya wa Taasisi hiyo Mh Edgar Kelvin (Wa kwanza kulia) na Aliyekuwa Mwenyekiti Wa UChaguzi Wa Kwanza Kushoto